Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, katika dini tukufu ya Kiislamu, matukio ya kidini yana nafasi maalumu, na kuheshimu hadhi ya masiku haya ni miongoni mwa majukumu muhimu kwa waumini, miezi ya Muharram na Safar inatambulika kama miezi ya maombolezo ya Bwana wa Mashahidi (as) na watu wa Nyumba ya Mtume (saw), na imekuwa na nafasi maalumu kwa Mashia. Katika kipindi hiki, baadhi ya matendo na mienendo huenda ikapingana na heshima ya nyakati hizi, jambo ambalo linahitajia ufafanuzi wa kina wa hukumu za kisheria.
Mtukufu Ayatollah Khamenei amejibu istift'a kuhusu maudhui hii, na tunaiwasilisha kwenu kama ifuatavyo.
Swali:
Je, kufanya hafla ya kuposa, aqdi na ndoa katika miezi ya Muharram na Safar kisheria inajuzu?
Jibu la Mtukufu Ayatollah Khamenei (Mola amuhifadhi):
Kuposa, aqdi na ndoa katika miezi ya Muharram na Safar kwa asili yake haina pingamizi lolote, lakini inapaswa kuepuka kufanya sherehe yoyote ya furaha ambayo katika desturi na mazoea ya kijamii itahesabiwa kuwa ni kuyavunjia heshima masiku haya ya maombolezo.
Chanzo: Tovuti rasmi ya Ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi (LEADER.IR)
Maoni yako